27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

KILI  STARS YAIPELEKA NUSU FAINALI KENYA

NA MWANDISHI WETU-MACHAKOS


TIMU ya soka ya Tanzania Bara  ‘Kilimanjaro Stars’ imeondolewa kwa aibu katika michuano inayosimamiwa na Baraza la Vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’ baada ya kukubali kichapo kingine cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’.

Kilimanjaro Stars imeondolewa katika michuano hiyo ikiwa iinashika mkia katika kundi lake A  baada ya kujikusanyika pointi moja,kupitia michezo minne, ikitoka sare mchezo mmoja na kuruhusu kufungwa michezo mitatu.

Katika mchezo wa jana dhidi ya Kenya, Kiliman jaro  Stars ilicheza soka lisilokuwa na ladha na kuiruhusu bao  dakika ya 19 kupitia kwa Vincent Ouma Oburu, baada ya beki wa Kilimanjaro Stars,Kenedy Wilson kuchelewa kupokea mpira wa pasi na matokeo yake kuwahiwa na mfungaji.

Bao hilo lilidumu hadi dakika 45 za kwanza zilipomalizika,kipindi cha pili mambo yalibadilika huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.

Mara kadhaa mashuti ya mshambuliaji wa Kilimanjaro Ibrahim Ajib, yaliokolewa na  kipa wa Kenya, Patrick Matasi.

Kadri muda ulivyosonga Kenya walizidisha mashambulizi langoni mwa Kilimanjaro Stars yaliyowaongezea  presha vijana wa kocha, Ammy Ninje ambao walionekana kupokonywa mipira kirahisi na wapinzani wao hao.

Katika mchezo huo,Ninje alifanya mabadiliko kadhaa kwa kuwaingiza chipukizi, Yahaya Zayd na Aman Kyata, lakini hawakuweza kutengeneza nafasi yoyote ya kuweza kupata bao la kusawazisha.

Kwa matokeo hayo sasa Kenya anaungana na Zanzibar kutinga hatua ya nusu fainali, licha ya Zanzibar kupoteza mchezo wake dhidi ya Libya kwa bao 1-0.

 

Ushindi huo uliifanya Libya kufikisha pointi sita,lakini haukuisaidia isiondolewe katika michuano hiyo baada ya kuzidiwa pointi moja na Kenya ambayo ilifikisha pointi saba kutokana na ushindi wake dhidi ya Kilimanjaro Stars. 

Kutoka kundi B, Uganda na Burundi zimefuzu nusu fainali ya michuano hiyo,hivyo kuungana na Zanzibar Heroes na wenyeji Kenya.

Ratiba ya fainali inaonyesha kuwa nusu fainali ya kwanza itachezwa Desemba  14, ambapo Kenya watacheza na Burundi, wakati nusu fainali ya pili itafanyika desemba 15, ambapo Uganda watacheza na Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles