27.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

KIKWETE: CCM INAPENDWA

Pg 1Bakari Kimwanga, Dodoma

MWENYEKITIwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amesema chama hicho bado kinapendwa na ndiyo maana mwaka huu wamejitokeza kugombea nafasi za ubunge na uwakilishi.

Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ta Taifa (NEC), jana jioni mjini hapa,  alisema “Tunakutana hapa leo hii (jana), kumaliza kazi iliyobaki ya uteuzi wa wanachama waliomba nafasi za ubunge, uwakilishi na ubunge na uwakilishi wa viti maalumu ili kukamilisha kazi ya wanachama wanaoomba nafasi za dola.

“Waliomba ni wengi sana ingawa inaonekana katika Chama Cha Mapinduzi kuna mvuto mkubwa kwa hiyo tuna kazi kubwa lakini kazi tuliofanya kwenye maadili na Kamati Kuu itasaidia kumaliza kazi kwa wakati,” alisema Rais Kikwete

Hata hivyo katika kikao hicho Rais Kikwete alihoji wajumbe wa NEC waliogombea ubunge ambapo idadi kubwa ya walionyoosha mikono ilikuwa kubwa hali ilimshangaza.

“Hee wajumbe wote wanagombea ina maana tumebaki mimi mzee Mangula na Kinana kazi kwelikweli….,” alisema Mwenyekiti huyo wa CCM huku akiangua kicheko

Awali akitoa taarifa za wajumbe waliihudhuria katika kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alisema kuwa wajumbe wote ni 374 na waliohudhuria 362 sawa na asilimia 96.

Katika kikao hicho cha NEC wajumbe watapitisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-20.

Magufuli ahudhuria

Katika kikao hicho mbali na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa chama na Serikali mgombea urais wa chama hicho Dk. John Magufuli naye alihudhuria na kushangiliwa na wajumbe na mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles