24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mbowe kumtambulisha Lowassa Mbeya kesho

lowassa na mboweNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kitengo cha moyo alipokuwa amelazwa kwa saa 48.

Kutokana na afya yake kuimarika, kiongozi huyo wa upinzani kesho anatarajiwa kushiriki katika mkutano wa kumtambulisha mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa, utakaofanyika jijini Mbeya.

Mbowe aliyehudumiwa na jopo la madaktari nane baada ya kushindwa kuhitimisha maandamano ya kumsindikiza Lowassa aliyeenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuchukua fomu alibainika kuwa na ugonjwa ambao kitaalamu unaitwa Fatigue (Fatiki), unaotokana na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.

Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene, jana alilieleza gazeti hili kuwa jopo la madaktari limemruhusu Mbowe kutoka hospitali baada ya kuridhika na maendeleo ya afya yake.

“Mwenyekiti ameruhusiwa baada ya madaktari kuona afya yake inaendelea vema na anatarajiwa kuendelea kufanyakazi za chama ikiwamo kumtambulisha mgombea urais wa chama chetu (Lowassa) kwenye mkutano utakaofanyika Mbeya,” alisema.

Juzi Dk. Tilizo Sanga, ambaye ni mmoja wa madaktari bigwa wa moyo waliomuhudumia Mbowe,  alisema maradhi hayo yanayotokana na uchovu unaochangiwa na mtu kufanyakazi kwa muda mrefu bila mapumziko ikiwamo kula chakula kidogo.

Dk. Sanga aliwaeleza waandishi wa habari kwamba Mbowe alipokewa hospitalini hapo Agosti 10, baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya TMJ Mikocheni.

Mbowe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema matatizo yake yamechangiwa na  kufanya kazi kwa muda mrefu usiku na mchana bila kupumzika, hasa kutokana na hali ya mambo inayoendelea nchini ilichangia afanye kazi kwa saa 24.

Mbowe alipata matatizo hayo wakati alipokuwa kwenye msafara wa kumsindikiza mgombea urais wa chama hicho, waziri mkuu wa zamani Lowassa kuchukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Viongozi waliomjulia hali   

Baadhi ya viongozi waliofika kumjulia hali na gazeti hili kushuhudia alikuwa ni Lowassa, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Wengine ni Mgombea Mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji, Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu.

Lowassa anakwenda Mbeya ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya ziara nje ya Dar es Salaam akiwa ndani ya vyama vya upinzani ambapo anatarajiwa kupata mapokezi makubwa naya aina yake.

Mapokezi ya Mbeya yanasubiriwa kwa hamu na wapenzi, mashabiki wa vyama hivyo hasa baada ya kutikisa jiji la

Dar es Salam kwa maandamano ya aina yake wakati alipokwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia Ukawa chini ya Chadema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles