25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

KIKAPU CHAMKUTANISHA JOKATE, CHAKACHAKA

MREMBO na mjasiliamali ambaye pia ni balozi wa kujitolea wa Mpira wa Kikapu ndani na nje ya nchi, juzi alikuwa alijiachia na wakongwe wa muziki barani Afrika, Yvonne Chakachaka na Olivia Mtukudzi katika sherehe ya Siku ya Wakongwe Afrika (Legends Night) uliofanyika jijini Johanesburg, Afrika Kusini.

Jokate ambaye alikuwa nchini humo kushuhudia mechi ya NBA Africa, ameliambia Show Biz kuwa Yvonne Chakachaka na Mtukudzi walialikwa kutumbuiza katika sherehe hiyo ya kuufurahia uafrika iliyojumuisha vyakula, mavazi na muziki wa zamani kutoka Afrika.

“Kama unavyojua kuna game ya NBA Africa kwa hiyo jana  kulikuwa kuna siku ya malengend Afrika na Chakachaka na Olivia Mtukudzi walialikwa tukutumbiza tukisherherekea uafrika wetu,” alisema Jokate.

Naye Yvonne Chakachaka katika moja ya picha alizoweka akiwa na Jokate katika mtandao wa Instagram alisema, “My new found daughter @jokatemwegelo, I am proud of you #forbes30under30,” kuonyesha kumkubali mrembo huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles