27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI YAMSHIKILIA MWANASIASA WA UPINZANI

LUSAKA, ZAMBIA

JESHI la Polisi nchini Zambia linamshikilia kiongozi wa chama kidogo cha upinzani cha United Progressive Party (UPP), Savior Chishimba, ambaye ameonekana kuwa mkosoaji namba mbili wa Rais Edgar Lungu.

Chishimba alikamatwa siku ya juzi muda mfupi baada ya kukamilishwa mahojiano ya moja kwa moja kwenye studio ya kituo cha Televisheni binafsi mjini Lusaka.

Huyu atakuwa ni mpinzani wa pili kukamatwa baada ya kinara wa upinzani nchini humo  Hakainde Hichilema, hatua inayochukuliwa na wanaharakati kuwa ni njama za kutaka kuuminya upinzani nchini humo.

Hivi karibuni Hichilema alisema kwa kipindi chote hicho amekuwa akipitia kipindi kigumu kwa sababu haki zake za msingi zinakiukwa na amezuiwa katika mazingira mabaya.

Hichilema alikamatwa mapema mwaka huu baada ya msafara wake kuzuia msafara wa Rais Edgar Lungu.

Mwanasiasa huyo ameyakanusha madai hayo na kusema ni ya kisiasa, yanayotumiwa dhidi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles