27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kijana Bukoba amuua mke wa bosi wake kisha kumbaka

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Jeshi la polisi mkoani Kagera linamtafuta kijana, Pascal Kaagwa(22) kwa kosa la kumuua, Khadija Ismaili(29) ambae alikuwa mke wa Mwenyekiti wa Mtaa wa National Housing kata ya Rwamishenye kwa kumpiga na kitu butu maeneo ya kichwani upande wa kushoto na kumsababishia jeraha kubwa ambalo lilipesababusha kuvuja damu nyingi na kumsababishia kifo.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, mara baada ya kufariki duni kwa mwanamke huyo, kijana huyo alimbaka na baada ya kutekeleza tukio hilo alitokomea kusikojurikana.

Hayo yameelezwa leo Februari 14, 2023 na Kamanda wa Jeshi la polisi mkaoni Kagera, William Mwampaghale wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema mtuhumiwa huyo alitekeleza mauwaji hayo Februari 13, mwaka huu saa 12 jioni nyumbani kwa Mwenyekiti, Divid Dominic alimokuwa anaishi mtuhumiwa huyo.

Pia, Mwampaghale amesema kuwa muda mfupi baadae watoto wa marehemu walifika nyumbani na kukuta mama yao akiwa amelala chini akiwa tayari amefariki dunia ndipo walitoa taarifa kwa majirani ili wapatiwe msaada zaidi.

Marehemu alikuwa akiishi na mume na watoto wake pamoja na mtuhumiwa, ambaye alikuwa anawasaidia kazi za nyumbani kama sehemu ya familia hiyo.

Jeshi hilolimetoa wito kwa wananchi wote kuwa makini kutambua wasifu wa vijana hasa pale wanapo waajiri kuwasaidia katika shughuri zao mbalimbali na kuamua kuishia nao.

“Nitumie nafasi hii kutoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo mbalimbali vya uhalifu ikiwemo mauwaji, ubakaji nakujichukulia sheria mkononi kuacha mara moja na hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote wanaofanya hivyo vya kihalifu ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani,” amesema Mwampaghale.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles