23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TBA yapunguza bei za nyumba Magomeni Kota

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeendelea kusisitiza kuwa umetekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan la kupunguza bei za nyumba za Magomeni Kota.

Machi 23, mwaka jana Rais Dk. Samia wakati akizindua nyumba hizo aliutaka Wakala huo kupunguza gharama za uuzaji wa nyumba hizo kwani zipo juu.

Awali, nyumba hizo zilikuwa zikiuzwa kwa Sh milioni 74 kwa chumba na sebule, na Sh milioni 86 kwa vyumba viwili na sebule.

Februari 6, mwaka huu wakazi 644 wa Magomeni Kota waligomea kusaini mkataba wa kuanza kununua nyumba hizo, kwa madai kwamba bei waliyoletewa sio rafiki na haiendani na hali ya uchumi wao.

Hayo yameelezwa leo Februari 14,2023, jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Daudi Kandoro wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wakala huo kwa mwaka 2022-2023.

Mtendaji huyo amesema baada ya maagizo ya rais walikutana na timu ya watalaamu na kujadiliana namna ya kupunguza bei ya nyumba hizo.

Amesema nyumba ya chumba kimoja itauzwa kutoka Sh milioni 74.8 hadi Shmilioni 48 na ya vyumba viwili kutoka Sh milioni 86 hadi Sh milioni 56.9.

Amesema kutokana na maelekezo ya rais wameweza kuondosha Sh bilioni 18.2.

Mtendaji huyo amesema wamepunguza bei ya nyumba hizo mara baada ya kuondoa gharama za ardhi, maeneo jumuishi kama korido, mandhari ya nje, mashimo ya maji taka na vizimba vya taka ngumu vilivyokuwa vimejumuishwa awali.

“Timu imekubaliana deni litarudishwa kwa miaka 15 na miaka mitano watakaa bure lakini hakutakuwa na riba. Niseme hakuna sakata kwa upande wa wakala tunatambua umoja wa wanakota,” amesema Mtendaji huyo.

Kuhusu madai ya miradi kutekelezwa chini ya kiwango, Mtendaji huyo amesema jambo hilo sio la kweli na TBA ina wataalamu wa kutosha ambao wamekuwa wakitumia weledi katika kazi zao.

Kuhusu madai ya mradi wa Magufuli Hosteli kutokuwa na ubora amesema yaliyojitokeza ni bahati mbaya kutokana na kutokufungwa kwa Expension joint.

“Bado tuna changamoto ya watumishi mahitaji ni 811 ila waliopo ni 350 lakini tunashukuru Serikali imetupa kibali na tutaanza kuajiri. Ila bado tuna changamoto ya vifaa ikiwemo  upatikanaji wa kokoto,”amesema Mtendaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles