20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Samia aridhia kutoa msamaha wa riba ya malimbikizo

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ameridhia kwa mara nyingine kutoa msamaha wa riba ya malimbikizo ambapo ametoa nafuu ya kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba ya malimbikizo kuanzia sasa hadi Aprili 30, mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo Februari 14,2023 na Waziri wa Ardh,i Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula wakati akifungua mkutano wa pili wa wadau wa sekta ya Adhi nchini katika ukumbi wa mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema uamuzi huo umefikiwa kutokana na maombi mengi yaliyowasilishwa na wananchi, hivyo Dk. Samia ameendelea kutumia hekima na busara zake kuongeza muda tena.

“Naomba nichukue fursa hii kuwajulisha kuwa Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameridhia kwa mara nyingine tena, baada ya kuombwa na kuridhia kuongeza kipindi cha masamaha hadi mwezi Aprili, 2023,” amesema Mheshimiwa Waziri Dk. Mabula.

Mheshimiwa Wazir,i Dk. Mabula amesema kuwa hayo ni matokeo ya mkutano ya kwanza walioufanya Mei 23, 2022 ambapo katika mkutano huo wadau hao walipata fursa ya kutoa maoni, hoja na mapendekezo ya kuboresha utoaji hudumu katika sekta ya ardhi.

Amesema kupitia mkutano huo wa awali, wizara imeyafanyia kazi maoni na hoja za wachangiaji 53 kwenye maeneo makubwa 15.

Kufuatia hoja na maoni hayo, Waziri Dk. Mabula amesema wizara imeandaa Bango kitita, maoni, hoja na mapendekeO yaliyotolewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles