Kulwa Mzee, Dar es Salaam
Wakili wa Serikali kutok Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, amedai mahakamani kwamba wamemaliza kumhoji kigogo wa IPTL, Harbinder Sethi baada ya kuomba mahakamani kufanya hivyo.
Swai amedai hayo leo Alhamisi Novemba 8, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo inatajwa.
Alidai upelelezi wa kesi hiyo ya kutakatisha fedha inayomkabili Sethi na James Rugemarila haujakamilika isipokuwa walipata nafasi ya kumuhoji Sethi.
Swai aliomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kesi kutajwa na upelelezi unaendelea.
Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 22 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Watuhumiwa hao bado wanaendelea kusota rumande
Mwisho