25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali haijaweka ukomo wa idadi ya watoto wa kuzaa

SERIKALI imesema haijaweka ukomo  wa idadi ya watoto wa  kuzaa kwa wananchi wake  na badala yake wazae idadi ambayo wataweza kumudu kuwapatia mahitaji yote muhimu.

Kauli hiyo ilitolewa  bungeni jana na Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dk  Faustine Ndungulile wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Suzan Limo (Chadema),

Katika swali lake, mbunge huyo alisema Serikali imetoa mwongozo wa kuondolewa kwa uzazi wa mpango baada ya kauli ya Rais kutaka wananchi wazae  bila ukomo,

‘’Nini kauli ya Serikali  uzazi wa mpango uwepo au kuondoa  na kuacha watu wazae watakavyoweza?” alihoji.

Akijibu swali hilo, Naibu waziri huyo alisema hakuna mwongozo wowote uliotolewa na Serikali wa kuondoa uzazi wa mango.

Dk. Ndungulile alifafanua kuwa hoja ya rais  haikulenga kusitisha  uzazi wa mpango bali alitaka watu wazae kulingana na uwezo wao.

‘’ Kila mtu anatakiwa kuzaa huku akijua anatakiwa kuwa na uwezo wa kuwapatia mahitaji muhimu kama vile chakula na elimu na huduma nyingine za binadamu na sio vinginevyo’’ alisema.

Akiongeza  majibu ya swali hilo, Mwenyekiti wa Bunge  Najma Giga alisema: ‘’ Hata katika vitabu vya dini vimesema kuwa zaeni muongezeke muijaze dunia, hivyo kauli ya Rais ipo sahihi na majibi ya Serikali pia sahihi’’.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Kilolo Venance  Mwamoto ( CCM) alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha k mkakati wa  taifa  wa  kupunguza vifo vya wanawake  na watoto  wa mwaka 2016 hadi 2020  unatimia.

“Tanzanai inakusudia kuongeza matumizi ya njia ya kisasa ya uzazi wa mpango  kutoka asilimia 32 ya mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 45 ifikapo 2020.

“Vilevile  kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi  kutoka 556 kwa kila vizazi hai 100,000 ya mwaka 2015 hadi 292 kwa kila vizazi hai 100,000 ifikapo 2020,

Akijibu swali hilo, naibu waziri alisema wizara  inatekeleza  mkakati wa pili wa kuboresha huduma za afya uzazi, mama, watoto na vijana  wa mwaka 2016 hadi 2020.

‘’ Mkakati huu umujikita zaidi kutekeleza malengo endelevu ya maendeleo ( SDGs) duniani na mkakati wan ne wa sekta ya afya,’’ alisema.

Alisema mkakati huo umeeleza bayana kuwa ili kupunguza vifo inahitaji kuhamasisha matumizi ya uzazi wa mpango , matumizi  mazuri ya wataalam wa uzazi (wakunga na madaktari).

Pia alisema  uwepo wa huduma za dharura za uzazi  na mtoto mchanga   na kuwa na mazingira yaliowezeshwa katika utoaji huduma.

Hata hivyo alisema wizara yake imeendelea kuboresha huduma bora ya dharula za uzazi na mtoto mchanga zenye uwezo wa kufanya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni, kwa kuzisogeza karibu na wananchi.

Alisema katika kuhakikisha hilo linafanikiwa tayari ujenzi na ukarabati wa vituo 208  unaendelea nchi nzima.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles