24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kiduku, Kabangu wachimbana mkwara uso kwa uso

Na mwandishi wetu, Mtanzania Digital

BAADA ya kila mmoja kutamba akiwa kwao siku za nyuma, mabondia Twaha Kiduku na Alex Kabangu leo wamekutana kwa mara kwanza kila mmoja akimchimba mkwara mwenzake kuelekea katika pambano la ubingwa wa UBO Afrika linalotarajia kupigwa Jumamosi Machi 26,2020 mkoani Morogoro.

Kiduku na Kabangu watapanda ulingoni katika pambano hilo la raundi nane katika uzito wa kati kwenye ukumbi wa Tanzanite chini ya kampuni ya Peak Time Media inayoongozwa na Meja Seleman Semunyu.

Akizungumzia maandalizi yake amesema mpinzani wake kaongea yote lakini yeye amejiandaa vizuri na kuwaondoa hofu Watanzania.

“Mimi nimefurahi kwa kuona kwamba kwa asilimia kubwa pambano lipo kwa sababu mpinzani kafika, afya yake ipo vizuri na mimi nipo vizuri,” amesema Kiduku.

Alex Kabangu

Naye Kabangu ametamba kuwa pambano hilo kwake ni kama anapasha kwa sababu anajiamini ndiye bondia bora Afrika katika uzito wa kati.
Kwa upande wake Mratibu wa pambano hilo, Bakari Khatibu amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100, huku akiwataka wadau wa ngumi nchini kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya masumbwi.

“Maandalizi kwa upande wetu ni mazuri tunashukuru Mungu tayari Kabangu ameshaingia na yupo hapa Morogoro, tunachosubiria ni siku hiyo kufika kwa ajili ya mambo mengine.

“Lakini nitume nafasi hii kuwashukuru wadhamini wote katika pambano hili ambalo linaenda kuacha historia kubwa ndani ya Morogoro, jambo la kuwakumbusha ni kwamba tiketi zimebakia chache hivyo watu waendelee kujitokeza kununua katika vituo,” amesema Khatibu.

Kiingilio katika pambano hilo ni sh 10,000, Sh 20,000 na Sh 30,000 kwa VIP.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles