24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

KIBATALA AJITOA KESI YA WEMA SEPETU

Na MANENO SELANYIKA-DAR ES SALAAM


WAKILI wa msanii maarufu wa filamu nchini, Wema Sepetu, Peter Kibatala, ameiandikia barua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,   Dar es Salaam,   kuomba kujitoa kumwakilisha katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.

Wakati huo huo mahakama imepokea barua kutoka kwa Wakili Albert Msando kuomba kumwakilisha msanii huyo katika kesi hiyo.

Msando  aliomba apewe muda wa kupitia jalada hilo kabla ya kuendelea na kesi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, alisema   alipokea barua hizo juzi   na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa    Februari 4, mwaka jana katika makazi ya Wema yaliyopo Kunduchi Ununio  Dar es Salaam, washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipande vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Naye Wema  anadaiwa kuwa Februari Mosi, mwaka jana katika  eneo lisilojulikana  Dar es Salaam,  alitumia bangi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles