27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

KESI ZA KODI ZAMTESA MAGUFULI, ASIMAMISHA WAKURUGENZI WAWILI

Na Anna Potinus, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amewasimamisha kazi wakurugenzi wa Wilaya mbili za Kigoma Ujiji na Pangani kutokana na wilaya zao kupata kuwa na hati chafu huku akiwataka majaji kuangalia namna ya kutatua kesi za kodi zilizofikia Sh trilioni 4.4.

Rais Magufuli amewasimamisha wakurugenzi hao leo wakati akipokea ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad ambayo pamoja na mambo mengine imezungumzia mafanikio na mapungufu katika sekta mbalimbali ikiwamo kesi za kodi.

“Wenyeviti wa Kamati ya Bunge wamenieleza niwe ninachukua hatua hivyo nimeanza kufanya kazi na hii inaweza kuwa ni fundisho kwa watu wengine,” amesema Rais Magufuli.

Akizungumzia suala la kesi za kodi, Rais Magufuli amemtaka Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Jaji Kiongozi, Ferdinand Wambali kukaa kwa pamoja na na kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo ambapo kesi zaidi ya trilioni 4.4 hazijatatuliwa wakati serikali bado inahitaji fedha.

“Ninafahamu mna upungufu wa majaji na mimi ninaendelea kuangalia namna ya kuwaongezea nguvu maana naweza nikateua majaji halafu nikakosa fedha za kuwalipa kwa sababu kuna trilioni 4.4 hivyo ninaomba unisaidie katika suala hili ili tuweze kuokoa fedha hizo zitusaidia kati mambo mengine,” amesema Magufuli.

Aidha, amewaomba viongozi wa serikali na Watanzania kwa ujumla kuungana kuitengeneza Tanzania mpya kwa kuwaasa kila mmoja kusimamia eneo lake ili nchi iweze kufika mbali.

“Nafahamu suala la bajeti ni gumu na linatesa kwani hata mimi nilipokuwa Waziri wa Ujenzi nilikuwa nikiandika barua kwa Rais Kikwete kuomba fedha za makandarasi ambazo hadi sasa bado nadaiwa,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles