25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya Mbowe, Matiko yapigwa kalenda

Na PATRICIA KIMELEMETA-DAR ES SALAAM

WAKATI Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, wakizidi kusota rumande, wakili wao, Profesa Abdallah Safari amehoji kuhusu rufaa iliyokatwa na upande wa mashtaka katika Mahakama ya Rufani.

Mbowe na Matiko wanasota mahabusu kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana November 26, mwaka jana kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Wakili Profesa Safari alitoa hoja hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi kuieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Kadushi alieleza kuwa, kuna amri ya kusitisha mwenendo wa kesi hiyo mpaka rufani itakaposikilizwa katika Mahakama ya Rufaa.

Baada ya kueleza hayo, Profesa Safari alimuhoji Wakili Kadushi kuwa rufaa iliyokatwa ilikuwa chini ya hati ya dharura? na kama hawakufanya hivyo ni kwa nini?.

Hata hivyo, Wakili Kadushi alijibu kuwa hakuna uhalali wa kisheria kuhusu swali hilo mahakamani hapo, labda lingeulizwa Mahakama Kuu ama ya Rufaa.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Januari17, mwaka huu huku akisema swali hilo la rufaa wakalihoji Mahakama Kuu.

 Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya  na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu 

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka huu maeneo ya  Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles