28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatenga bil. 22 mradi wa maji Tanga

Amina Omary, Tanga

Serikali inatarajia kupeleka kiasi cha Sh bilioni 22 kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya maji katika wilaya za Pangani, Muheza na Korogwe.

Hayo yamesemwa na  Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo, wakati akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Tanga mara baada ya kupatiwa taarifa ya maendeleo ya sekta ya maji mkoani humo leo Ijumaa Januari 4.

Amesema fedha hizo zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kukamilisha miradi ya awali lakini pamoja na kuanza miradi mipya.

“Tunaratajia miradi hiyo katika wilaya hizo kuanza katika kipindi cha kuanzia Septemba, nia ya serikali ni kuhakikisha huduma ya maji inawafikia Watanzania wote katika maeneo yao ili kuhakikisha wanaondokana na changamoto ya ukosefu wa huduma hiyo,” amesema.

Awali akitoa taarifa ya Mkoa wa Tanga, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Zena Said, alisema sekta hiyo inakabiliwa na changamoto za malimbikizo ya madeni ya huduma ya maji kutoka taasisi za serikali na madeni ya wazabuni ambao wanatekeleza ujenzi wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, amemuomba katibu mkuu huyo kuwasaidia huduma ya maji katika Wilaya ya Mkinga ambayo kwa sasa ina changamoto kubwa ya uhaba wa huduma hiyo.

“Tulikuwa tunaomba msaada maalumu kwa Wilaya ya Mkinga kupatiwa huduma ya maji hasa maeneo mawili ambayo ni maalumu, makao makuu ya wilaya pamoja na eneo la mpakani Horohoro,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles