24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya Kafulila yarudi tena mahakamani

david-kafulilaNa Mwandishi Wetu

RUFAA ya Kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini kati ya David Kafulila (NCCR-Mageuzi) dhidi ya Hasna Mwilima (CCM), iliyotolewa na Jaji Ferdinand Wambali, ilitenguliwa Oktoba12, mwaka huu, baada ya mapingamizi yaliyowekwa na upande wa mawakili wa Serikali kwamba hati ya mashtaka ilikuwa na kasoro za kiufundi imerudishwa tena mahakamani.

Kutokana na kasoro hiyo, mawakili wa Serikali waliomba Mahakama ifute moja kwa moja rufaa hiyo (dismiss), ingawa majaji wa mahakama ya rufaa wakiongozwa na Jaji Bernard Luanda,  Salim Mbarouk na Jaji Richard Mziray, waliamua kutengua hati hiyo  kwa namna ambayo Kafulila angeweza kurejesha rufaa hiyo, baada ya kurekebisha kasoro tajwa kwa hoja kwamba Mahakama haiwezi kuifuta moja kwa moja wakati haijafikia kusikiliza hoja za msingi wa rufaa husika.

Kutokana na uamuzi huo, Kafulila aliomba Mahakama kurekebisha kasoro hizo ili kesi ya msingi isikilizwe kuamua nani aliyeshinda uchaguzi wa jimbo hilo Oktoba 25, mwaka jana kwa mujibu wa fomu za matokeo 21B ambazo ziliwasilishwa na NEC mahakamani, huku kila upande ukidai umeshinda.

Baada ya Kafulila kufikisha maombi hayo, mahakama jana imeagiza pande husika na kesi kufika mbele ya Jaji Emmanue Mrangu Novemba 3, mwaka huu mjini Tabora, kwa ajili ya ombi hilo lililowasilishwa na Kafulila ili rufaa iweze kuendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles