28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya Eva, Mourinho kunguruma Machi

Eva-Carneiro-010LONDON, ENGLAND

KESI ya kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho na aliyekuwa daktari wa timu hiyo, Eva Carneiro, inatarajiwa kusikilizwa Machi 7, mwaka huu.

Mgogoro wa Mourinho na Eva ulianza tangu Agosti mwaka jana, katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu kati ya Chelsea na Swansea City, ambapo mchezo ulimalizika kwa sare ya 2-2.

Mourinho alimtupia lawama daktari wa timu hiyo, Eva, kwa kutumia muda mrefu kumtibu mshambuliaji wao, Eden Hazard, wakati timu yao ikionekana kuwa na nafasi ya kupata bao la tatu. Kutokana na hali hiyo, Mourinho alimtupia maneno ya kibaguzi daktari huyo na kumsimamisha kazi.

Hata hivyo, klabu ya Chelsea baada ya muda ilimuomba Eva kurudi kazini, lakini alikataa na aliamua kumfungulia mashtaka kocha huyo kutokana na maneno ya kashfa.

Kesi ya wawili hao inatarajiwa kusikilizwa Machi mwaka huu, huku wote wakiwa hawana kazi, Mourinho alifukuzwa na klabu kutokana na matokeo mabaya na Eva tangu afukuzwe na klabu hiyo hajarudi viwanjani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles