27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Keane: Toure ni hatari akiamua

Roy-KeaneMANCHESTER, ENGLAND

KIUNGO wa zamani wa klabu ya Manchester United, Roy Keane, amedai kwamba nyota wa Manchester City, Yaya Toure, ni mchezaji hatari pale anapoamua kujitolea kwa ajili ya timu yake.

Juzi klabu ya Man City ilishuka dimbani kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev, ambapo City ilifanikiwa kushinda mabao 3-1, huku Toure akifunga bao moja na akitoa mchango mkubwa katika ushindi huo.

Akizungumza wakati wa uchambuzi wa mchezo huo na kituo cha ITV nchini England, Keane alisema kwamba kiungo huyo raia wa Ivory Coast, anakuwa na mchango mkubwa pale akiamua kuitafutia bao timu yake.

“Kuna wakati Toure uwanjani anachosha, lakini pale anapoamua kuibeba timu utafurahia kuona kile ambacho anakifanya, kwa kuwa anazunguka uwanja mzima na kulazimisha bao.

“Tumemuona katika mchezo dhidi ya Dynamo Kiev, ameonesha uwezo wake na ndivyo inavyotakiwa mchezaji kujituma ili kuipa ushindi timu,” alisema Kaene.

Ushindi huo wa juzi, unawapa nafasi kubwa ya kuingia hatua ya robo fainali katika michuano hiyo huku wakisubiri mchezo wa marudiano ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Etihad.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles