30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wakala akanusha Gareth Bale kuuzwa

gareth baleMADRID, HISPANIA

WAKALA wa mshambuliaji wa timu ya Real Madrid, Gareth Bale, Jonathan Barnett, amekanusha uvumi wa kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kuuzwa wakati wa majira ya joto kutokana na kuwa na majeraha ya mara kwa mara.

Inadaiwa kwamba mchezaji huyo amekuwa na majeraha ya mara kwa mara tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Tottenham mwaka 2013 kwa kitita cha pauni milioni 85.3, hivyo mchango wake umekuwa mdogo ndani ya klabu hiyo.

“Hizi ni habari za kijinga ambazo zinasambazwa na watu wenye mitazamo yao binafsi, hakuna ukweli wowote juu ya habari hizo, bado ataendelea kuwa mchezaji wa klabu hiyo hadi pale mwisho wa mkataba wake,” alisema Barnett.

Bale, mwenye umri wa miaka 26, kwa sasa ni majeruhi na kuna uwezekano mkubwa wa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania kesho dhidi ya Atletico Madrid, mchezo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.

Hata hivyo, mchezaji huyo kwa sasa ana jumla ya mabao 13 katika michezo 15 ya Ligi Kuu nchini Hispania msimu huu, huku akitoa pasi nane za mwisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,396FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles