27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kerr awakomalia Mgosi, Ajibu

kocha_mpya_simbaNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, ameanza kuwanoa washambuliaji wa timu hiyo na kuwapa programu maalumu ili kuondoa tatizo sugu ya ubutu linalowasumbua kabla ya kuvaana na Azam FC Desemba 12, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Washambuliaji ambao kocha huyo raia wa Uingereza ameanza nao ni Mussa Hassan ‘Mgosi’, Boniface Maganga na Ibrahim Ajibu, huku akisisitiza kutaka idadi kubwa ya mabao kwenye mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo juzi katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kerr alisema anawapa mbinu washambuliaji wake ili kila mmoja aweze kujitengenezea mabao ya kufunga kutokana na kuwasoma vizuri wapinzani wao.

“Kwa sasa nimeanza na hawa waliopo kikosini, wakati nikiwasubiri wengine wanaozitumikia timu za Taifa kwenye michuano ya Chalenji, lakini watakaporejea nitawaunganisha na kuunda safu imara ya ushambuliaji ambayo itakuwa tishio ligi kuu,” alisema.
Kerr alisema anaamini programu hiyo itawasaidia kubadilika na kuendana na kasi ya ligi katika mechi zilizosalia mzunguko wa pili na kufanya kikosi hicho kiweze kuongoza katika msimamo na kuwashusha vinara Azam waliopo kileleni.
Kocha huyo aliwashauri viongozi wa Simba kujenga mazoea ya kuwatunza wachezaji wenye umri mdogo ambao wanaonekana kuwa na vipaji vya hali ya juu, ili baadaye waweze kuwatumia kuimarisha timu hiyo.

“Wachezaji kama Hassan Ramadhani ‘Kessy’, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Said Ndemla na Issa Abdallah wanahitaji kupewa ushirikiano zaidi ili kuendeleza viwango vyao kwani wanaweza kuwa hazina kubwa kwa klabu kwa kuwa umri wao bado ni mdogo,” alisema.

Katika mechi tisa ambazo Simba wamecheza ligi kuu, wamefanikiwa kushinda mara saba na kufungwa 2-0 na mahasimu wao Yanga kabla ya kupigwa bao 1-0 na Tanzania Prisons.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles