25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kenya, Tanzania kuondoa vikwazo vya kiutawala

Na Mwandishi Wetu

TANZANIA na Kenya zimedhamiria kumaliza vikwazo vya kiutawala vilivyosalia ifikapo Desemba 2021 baada ya kuondoa 46 visivyokuwa vya kikodi.

Kauli hiyo imetokana na mazungumzo  kati  ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dany Kazungu  jijini Dar es Salaam ambapo takwimu zinaonesha biashara kati ya nchi hizo umeongezeka mara sita zaidi baada ya kuondolewa kwa vikwazo hivyo.

Kwa mujibu wa wa taarifa iliyolewa  leo Oktoba 18,2021 na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kutokana na hatua hiyo, Tanzania imeonekana kunufaika na kuondolewa kwa vikwazo hivyo kwa kuuza zaidi bidhaa zake nchini Kenya.

“Hii ni ishara nzuri kwa Tanzania lakini pia ni fursa kwa Tanzania na Kenya kuondoa umaskini kwa watoto wetu na ndugu zetu kupata ajira kwa wingi katika sekta ya biashara,” amesema Balozi Kazungu

Mazungumzo  kati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Kenya nchini Tanzania,Dany Kazungu katika Ofisi ndogo za wizara leo Jijini Dar es Salaam

Balozi huyo amemueleza Waziri Mulamula kuhusu azima ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kufanya ziara rasmi hapa nchini na kisha kuhudhuria sherehe za Uhuru Desemba 9,2021 ambapo alialikwa na Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea Kenya mapema mwaka huu.

Kwa upande wake Waziri Mulamula amesema Tanzania inaheshimu makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa awali wa kuondoa vikwazo hivyo na  lengo ni ni kuwa ifikapo Desemba 2021 vikwazo vya kiutawala navyo viwe vimeondolewa ili kukuza zaidi mahusiano ya Kidiplomasia na biashara baina ya Tanzania na Kenya.

“Tumekubaliana kuhakikisha ifikapo Desemba 2021 vikwazo vyote vya kitawala viwe vimetatuliwa azma yetu ni kuhakikisha kuwa kila kitu kinakuwa sawa kwa ustawi wa Diplomasia na biashara baina ya Tanzania na Kenya,” amesema Balozi Mulamula.

Mwakilishi wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani, Ronda Pierce (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam

Wakati huo huo, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na mwakilishi wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani, Ronda Pierce katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles