23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

KENYA KINARA ULIMBIKIZAJI MADENI

dollars_flying_flickr

NAIROBI, KENYA

KENYA inaongoza miongoni mwa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa limbikizo la deni, ikifuatiwa na Tanzania, Rwanda na Uganda, imesema ripoti mpya ya tathmini.

Katika mwaka wa fedha 2016/2017, Kenya imepanga kukopa dola milioni 600 kutoka kwa wakopeshaji wa kigeni, kuwezesha bajeti yake ya miradi ya maendeleo na kujaribu kuziba pengo la kifedha linalofikia dola bilioni 5.38 katika mwaka wa sasa wa fedha.

Mgawo wa deni la umma la Kenya kwa uwiano wa pato la ndani (GDP) uliongezeka kutoka asilimia 41.7 mwaka 2012 hadi asilimia 55.4 mwaka 2016, wakati Tanzania lilikua kutoka asilimia 29.2 hadi asilimia 42.4 katika kipindi hicho.

Rwanda ilisimama katika asilimia 41.5 kutoka asilimia 20.1 na Uganda ilipanda hadi asilimia 37.9 kutoka asilimia 24.2 katika kipindi hicho cha tathmini.

Katika tathmini yake mpya iitwayo ‘Sub-Saharan Sovereign Debt Rises, Hampers Consolidation’, Taasisi ya Fitch Ratings imesema ongezeko hilo la deni lilichangiwa na kushuka kwa makusanyo ya kodi na kiwango kikubwa cha ukopaji kinachofanywa na Serikali katika kugharimia miradi ya miundombinu.

“Wakati uwekezaji wa miundombinu unaochangia haya madeni utasaidia kuondoa vikwazo katika ukuaji wa uchumi kwa mpango wa muda mrefu, faida zake zinaweza zisizae matunda yanayokusudiwa, hadi utawala bora na mazingira ya biashara yatakapoimarika,” ilisema taasisi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles