WAANDISHI ARUSHA WAGOMEA MKUTANO KUDAI UHURU WA MWENZAO

0
558
mwaandishi-arusha
Baadhi ya Wanahabari wakiwa Kituo cha Polisi USA Arusha wakifuatilia kukamatwa kwa Mwandishi Halfan Lihundi

Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha kwa umoja wao wamegoma kwenda ziara ya Waziri wa Ardhi William Lukuvi na badala yake wameelekea kituo cha polisi USA River kuhakikisha mwandishi mwenzao wa ITV Halfan Liundi anaachiwa huru.

Katika hilo, Azimio lililopitishwa ni kuwa wote kwa umoja wao watamtenga mwandishi yoyote atayehudhuria na kuandika kilichojiri kwenye mkutano huo wa Lukuvi.

Lihundi aliwekwa ndani na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti  akimtuhumu kuripoti taarifa ya maji ambayo hakuipenda na kuwa amekuwa akiandika habari za uchochezi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here