31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

WASANII MAJUU WALIOFANYA VIZURI/VIBAYA 2016

Justin Bieber Performs At KeyArena

Na BADI MCHOMOLO,

TUKIWA tunakaribia kumaliza mwaka 2016 na kukaribisha mwaka 2017, wapo wasanii wa nje waliofanya vizuri na waliofanya vibaya katika kazi zao za muziki kwa mwaka huu.

Adele Adkins

Mwaka huu kwake umekuwa wa mafanikio makubwa kutokana na wimbo wake wa ‘Hello’ uliotoka mwishoni mwa mwaka jana.

Wimbo huo wa raia huyo wa Uingereza mwenye miaka 28, umeweka historia kwa kuuza zaidi ya kopi milioni 3.38 ndani ya wiki moja, historia hiyo iliwahi kuwekwa mwaka 1991 na mwanamuziki, Nielsen SoundScan.

Kwa mwaka huu wimbo huo umemwingizia zaidi ya dola milioni 80.5 kwa mwaka, fedha ambazo hazijafikiwa na msanii mwingine.

Justin Bieber

Nyota huyu wa muziki wa Pop kutoka Canada anayefanyia shughuli zake nchini Marekani, mwaka huu ameng’aa kutokana na albamu yake ya ‘Purpose’ kufanya vizuri licha ya kuitoa mwishoni mwa mwaka jana.

Nyimbo zilizotamba katika albamu hiyo ni ‘What Do You Mean?’,  ‘Love Yourself’  na ‘Sorry’ nyimbo ambazo zilimwezesha Bieber kunyakua tuzo nne kwenye tuzo za American Music Awards.

Aubrey Drake

Ni rapa kutoka kundi la Young Money Cash Money Records. Kwa mwaka huu Drake amefanya vizuri kuliko wasanii wenzake kwenye kundi hilo kiasi cha kumwezesha kuzoa tuzo tatu za American Music Awards sawa na tuzo alizopata mpenzi wake Rihanna.

Drake alikuwa akigombea tuzo hizo kwenye vipengele 13 na kuandika historia mpya baada ya kuwahi kushikiliwa na aliyekuwa mfalme wa pop duniani, Michael Jackson (marehemu) ambaye mwaka 1984 aliyewahi kuwa kwenye vipengele 11.

Wizkid

Msanii huyu wa Nigeria mwaka huu amefanya vizuri kiasi cha kuwashawishi wasanii wanaotamba katika muziki duniani, akiwemo Chris Brown na Drake kufanya naye kazi.

Drake alirudia wimbo wa msanii huyo wa ‘Ojuelegba’ na Brown alimpa nafasi ya kufanya naye shoo mbalimbali katika nchi za bara la Ulaya na shoo yake ya Afrika Mashariki alipotua nchini Kenya alifanya na msanii huyo shoo hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mombasa Golf Club ambayo iliwanufaisha na wasanii kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania iliyowakilishwa na wasanii wake wawili, Vanessa Mdee na Ali Kiba.

Utajiri

Licha ya kutokufanya vizuri katika muziki, wasanii hawa wa hip hop wana utajiri mkubwa unaotokana na kazi zao za muziki na biashara zao mbalimbali zikiwemo lebo za kampuni zao za muziki, biashara ya vinywaji ‘pombe’, lebo za mavazi yao, headphones na mikataba mbalimbali ya makampuni ya kibiashara.

Anayeongoza ni P.Diddy aliyetajwa na jarida la Forbs akiwa na utajiri wa dola za Marekani milioni 650, Jay Z anafuatia akiwa na utajiri wa dola milioni 550 huku Dr. Dre akishika nafasi ya tatu kwa kuwa na dola milioni 450.

Master P wa nne akiwa na milioni 350 huku 50 Cent na utajiri wake wa dola milioni 270 akishika nafasi ya tano.

Ja Rule

Rapa huyu baada ya kutokufanya vizuri miaka kadhaa, ametangaza kufikiria kuachana na muziki na kujikita katika biashara zake nyingine ikiwemo uandaaji na uchezaji wa filamu.

Kandric Lamar

Mwaka huu msanii huyo ameshindwa kuwika kama alivyoweza kuwazima waliokuwa wakimpinga kutumia jina la ‘King of hip hop’ baada ya kung’ara mwaka 2013/2014 na kunyakua tuzo kadhaa.

Lil Wayne

Alisumbua sana kimuziki miaka ya nyuma akiwa na staili yake ya kujichora mwili mzima, lakini mwaka huu ameshindwa kuwika kutokana na kuingia kwenye mgogoro na bosi wake, Birdman na kujitoa katika kundi hilo la Cash Money akitaka alipwe dola za Marekani milioni 51 anazodai zilitokana na kulifanyia kazi kundi hilo lakini hakulipwa hadi leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles