24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KCB yawakumbuka watoto yatima

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Benki ya KCB imetoa msaada wa vyakula katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Center kilichopo Hananasifu, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Vyakula hivyo ni mchele, maharage, mafuta ya kupikia, tambi, sukari, chumvi na unga wa ngano venye thamani ya Sh milioni 2.3.

Akizungumza na Dar es Salaam leo Aprili 5, 2023 mara baada ya kukabidhi msaada huo Mkuu wa mahusiano wa Benki hiyo, Christina Manyenye amesema lengo la kufanya hivyo ni kuwajali watoto wenye hao wenye uhitaji katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Benk yetu inatambua umuhimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kufanya mema na kwakutambua umuhimu huo tumeamua kurudisha kwa jamii ambapo tumetoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa kituo hiki cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni Hananasif.

“Ikumbukwe kuwa kituo hiki kina zaidi ya watoto 30 hivyo tunaamini kuwa kwa hiki kidogo tulichokitoa kitasaidia katika mahitaji yao ya kila siku,” amesema Christina.

Ameongeza kuwa mbali na msaada huo benki ya KCB imeendelea kuwasaidia makundi mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana kupitia veta ili waweze kujiajiri na kuwasaidia Watanzania wengine.

“Tunaangalia upande wa wanawake pia kujikimu kuwafundisha waweze kuendesha biashara ambazo ni endelevu ambapo uzao wake utakuja kufaidika na kuchochea kupunguza watoto wa mitaani,” amesema.

Kwa upande Mkuu wa Huduma za Benki za Kiislamu –KCB Sahl Banking, Amour Muro, amesema benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa watanzania ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Naye, Mkuu wa Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Maunga Centre, Rashid Matimba ameishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema umekuja wakati muafaka.

“Tunaipongeza benk KCB kwa msaada wao, tunaomba benki zingine waige mfano wa benki hii,” amesema Matimba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles