23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

UDSM yazindua kitabu cha ushirikiano wa wadau wa uhifadhi

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Sayansi za Jamii kimezindua kitabu kuhitimisha mradi wa ’Ushirikiano wa wadau mbalimbali katika Uhifadhi na Maendeleo ya Kiikolojia na Jamii’ New Conservation Partnerships for Sustainability (NEPSUS).

Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Christine Noe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho, amesema kuwa utafiti wao ulijikita kwenye Maliasili, Misitu na Mazao ya bahari.

“Tumeangalia upande wa jamii zinazopatikana karibu na misitu, kitabu kimesheheni mambo mhimu ya jamii na namna inavyofaidika uwepo wa maliasili zinazowazunguka pamoja na changamoto wanazokutana nazo,” amesema Christine.

Aidha, ameomba jamii zifikiwe na tafiti hizo ili kuweza kubadilisha hali ya kiuchumi za wananchi wanaozungukwa na maliasili husika mahali walipo.

“Machapisho ya kitaaluma tumefanya sasa yapo kwenye sehemu zinazotakiwa za kitaaluma lakini mapendekezo ya Serikali nini ifanye, tulitafuta wadau wa maliasili, wakurugenzi wa maliasili, wa misitu na uvuvi tukajadiliana nakuja na machapisho madogo ya kisera ili serikali iweze kubadilisha sera kulingana na maisha ya sasa,” amesema Christine.

Kwa upande wa Wahariri wa kitabu hicho, Dan Brockington kutoka Chuo Kikuu cha Autonomous Barcelona nchini Hispania amesema walifanya utafiti huo kwa ushirikiano mkubwa kati yao na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Tanzania inabahati ya kuwa na watafiti wengi wanaofanya kazi zao katika usimamizi wa maliasili kwa hiyo imekuwa ni rahisi kwao kufanya utafiti huo juu ya misingi mizuri ambayo ilikuwa imejengwa tayari,” amesema Brockington.

Amesongezea kuwa changamoto kubwa ni kulinganisha chanzo cha mapato kwa wananchi ni tofauti na maliasili inayopatikana katika eneo husika.

Amesema kama eneo la hifadhi ya maliasili limeongeza basi na kipato cha wananchi kiwe kizuri.

Kwa upande wake, Stefano Ponte kutoka Shule Kuu ya Biashara ya Copenhagen, amesema ushirikiano katika utafiti huo ulianza mwaka 2016 hadi 2020 ingawa yeye alikuwa na mawazo mengine katika utafiti huo.

Aidha, waliungana pamoja katika utafiti huo na sasa wanasheherekea uzinduzi wa kitabu hicho pamoja hii ni hatua kubwa kwani hata yeye amesema amejifunza kupitia utafiti huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles