23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

‘This Year Blessings’ yampaisha Victor Thompson

Lagos,Nigeria

Mwimbaji wa Injili kutoka nchini Nigeria, Victor Thompson, ameweka wazi kuwa wimbo wake This Year Blessings uliotoka mapema mwaka huu, umeendelea kumfungulia milango ya mafanikio.

Victor ambaye ni bosi wa lebo ya Atmosphere Ent, ameliambia www.mtanzania.co.tz kuwa wimbo huo umeendelea kufanyika baraka ndani na nje ya Nigeria kwa kugusa maisha ya watu.

“Ni wimbo uliofanyika baraka kwangu na kwa watu wengi ndani na nje ya Nigeria, hii imenipa nguvu zaidi ya kuendelea kufanya kazi ya Mungu,” amesema Victor.

Aidha, Victor ambaye ni mtunzi wa nyimbo, mwimbaji, kiongozi wa ibada amemshukuru mkewe Henrietta Thompson ambaye amekuwa akimtia moyo katika kutimiza kusudi lake la kuishi maisha yenye athari chanya kwa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles