MKALI wa nyimbo za injili nchini, George Kayala, amekamilisha albamu yake ya pili aliyoipa jina la ‘Maajabu ya Damu ya Yesu’.
Nyimbo hizo zilizopo katika albamu hiyo ni ‘Damu ya Yesu’ ambayo imebeba jina la albamu, ‘Kanitendea Mema’, ‘Fungua Njia’, ‘Dhihirisha Uwezo Wako’, ‘Wastahili Sifa’, ‘Umenikumbuka’ na ‘Tanzania’.
Albamu yake ya kwanza ya ‘Siwema’ nayo ilikuwa na jumla ya nyimbo saba. Kwa sasa mwimbaji huyo yupo katika maandalizi ya upigaji wa picha za video za nyimbo zake hizo.