29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Ray Kigosi atakiwa awe balozi wa maji

rayNA SUZANA MAKORONGO (RCT)

BAADA ya mwigizaji mashuhuri katika filamu, Vicent Kigosi ‘Ray’ kudai weupe wake unatokana na kunywa maji mengi na kufanya mazoezi na siyo mkorogo, makampuni manne yanayojishughulisha na masuala ya maji yamemtaka awe balozi wao.

Ray alisema licha ya makampuni hayo ambayo hakutaka kuyaweka wazi kujitokeza, bado hajawa tayari kwa sasa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ray alisema kubadilika kwake kwa ngozi kumeleta gumzo kubwa kwake na pia kumempatia neema kutokana na makampuni hayo kutaka awe balozi wao.

“Kunywa kwangu maji kwa wingi na kushiriki mazoezi ipasavyo ndiyo kumepekekea ngozi yangu kuwa nyororo na makampuni yaliyojitokeza kwa sasa nimewaambia wasubiri kwanza hadi nitakapokuwa tayari kuwa balozi wao,’’ alieleza Ray.

Katika hatua nyingine, msanii huyo wa filamu anatarajia kutoa filamu yake mpya ya ‘Tajiri Mfupi’, Februari 29. Filamu hiyo ina vichekesho na masuala mengine ya kuelimisha kupitia vichekesho.

“Kwenye hii ‘movie’ nataka watu wamuone Ray mwingine kabisa, nitawapa burudani ya nguvu na mjiandae kuvunja mbavu,” alisema.

Ray aliongeza kwamba soko la filamu kwa sasa limekuwa gumu kwa kuwa hakuna watu wa kuwekeza kwenye movie, pia kampuni kubwa ya usambazaji ipo moja, hivyo inazidiwa na kazi za wasanii ndiyo maana soko limekuwa la shida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles