27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kaya 6,000 Simiyu hazina vyoo

Derick Milton, Simiyu

Kampeni inayolenga kuhamasisha jamii kuwa na vyoo bora inayojulikana kama ‘Nyumba ni Choo’ imezinduliwa rasmi mkoani hapa huku ikidaiwa kaya 6,459 sawa na asilimia tatu, hazina vyoo.
Kampeni hiyo itaendeshwa kwa siku 20 ikiongozwa na msanii maarufu nchini, Mrisho Mpoto.


Kabla ya kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka, Katibu Tawala wa Mkoa Jumanne Sagini amesema mbali na hilo kaya 215,316 sawa na asilimia 97 ndizo zenye vyoo ambapo kati ya hizo zenye vyoo bora ni 97,536 sawa na asilimia 46.7 ya kaya zote.

“Katika kuhakikisha suala hilo linatiliwa mkazo mkoa umejipanga kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora kwa kila kaya ikiwa pamoja na kutiliwa kwa mkazo wa sera za usafi wa mazingira,” amesema.

Naye Mratibu wa Kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Anyitike Mwakitalima amesema kupitia kampeni hiyo wamelenga kuongeza uwepo wa vyoo bora kwa kipindi cha muda mfupi.


“Mbali na hilo kampeni hiyo itahakikisha inaboresha hali ya afya katika nchi sambamba na kukabiliana na uchafu kwa njia zote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ujenzi wa vyoo bora kwenye ngazi ya kaya na taasisi,” amesema.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema tatizo la kutokuwa na vyoo bora linasababishwa na baadhi ya tamaduni ambapo katika baadhi ya jamii baba mkwe hatumii choo kimoja na mkwe wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles