26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Wakulima Kagera watakiwa kuchangamkia fursa

RENATHA KIPAKA -KYERWA

BODI ya Kahawa mkoani Kagera, imetoa wito kwa wakulima kuchangamkia fursa ya kulima kilimo hai ili kuondokana na tatizo la masoko linalowakumba.

Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa bodi hiyo, Melkiol Massawe alipofika katika shamba la mkulima bora wa kahawa aina ya robusta lenye ekari zaidi ya 100 ili kuendelea kumpa elimu zaidi.

Alisema kilimo hai hakina usumbufu katika soko la dunia na la ndani  kutokana na kahawa kulimwa pasipo kutumia dawa  zilizo na sumu.

“Kahawa ya kilimo hai ambayo inalimwa kwa mkulima huyu (Albert Katagira) ni tofauti na inayolimwa na wakulima wengine wanaotumia mbolea ya sumu.

“Huyu anatumia mbolea ya asili ambayo ni nyasi, masalia ya migomba, mbolea ya samadi na mboji,” alisema Massawe.

Kwa upande wake, Katagira ambaye ni mkulima bora Tanzania kwa mwaka huu, alisema shamba alilonalo ni ekari 100 na ekari 50 tayari zimepandwa na kwa mwaka amevuna gunia 400.

Alisema ili kilimo kiweze kuleta manufaa, wakulima wanapaswa kuongeza bidii na kuzalisha malighafi nyingi ambazo zitamsaidia kujiongezea kipato.

“Nitumie nafasi hii kuwashauri wakulima wenzangu kulima kilimo cha kulinda afya zetu na kujiongeza kuanzisha viwanda ambavyo vitasaidia kuchakata malighafi itakayosaidia kuongeza thamani,” alisema.

Ofisa Kilimo wa Kijiji cha Ishaka-Iingiro, Elica Dario, alisema amekuwa akikagua shamba la Katagira ili kumsaidia elimu ya kilimo bora na kufuata maelekezo anayopewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles