24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kavumbagu, Morris waanza mazoezi rasmi

aggrey-morriskavuNA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka Burundi, Didier Kavumbagu na beki mahiri Aggrey Morris wa Azam FC, wameanza rasmi mazoezi baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakiwakabili.

Morris alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti tangu Novemba mwaka jana, alipoumia wakati akiwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’, iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji iliyofanyika nchini Ethiopia.

Mwezi uliopita mlinzi huyo alipelekwa jijini Cape Town, Afrika Kusini, katika Hospitali ya Afrisurb kufanyiwa matibabu ambapo alitakiwa kupumzika kwa takribani wiki tatu kabla ya kuanza mazoezi.

Kwa upande wake Kavumbagu, alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya enka aliyopata wakati wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi mwezi uliopita dhidi ya Yanga, uliofanyika visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, Juma Mwimbe, Morris ameanza na mazoezi ya gym ambayo atafanya kwa muda wa wiki moja, kabla ya kuhamia kwenye mazoezi mepesi ya uwanjani kwa muda wa wiki moja.

“Morris ameanza mazoezi ya gym ili aweze kuwa fiti zaidi kutokana na kukosa mechi kwa muda mrefu, lakini baada ya hapo atajiunga na wenzake uwanjani mara baada ya timu kurejea kutoka Mbeya, ambako tutacheza na Mbeya City na Tanzania Prisons,” alisema.

Mwimbe alisema Kavumbagu naye alianza mazoezi ya gym jana, ambayo atafanya kwa siku kadhaa kabla ya kuanza mazoezi na wenzake uwanjani.

“Programu ya Kavumbagu kabla ya kurejea uwanjani ni fupi kwa kuwa hajakaa nje muda mrefu,” alisema Mwimbe.

Kurejea dimbani kwa nyota hao, kutaleta manufaa kwa timu hiyo inayokabiliwa na michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho, ambapo Azam wamepangwa kuanzia raundi ya kwanza mwezi ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles