23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Beki Ulinzi Stars auawa Somalia

Kevin-Ouma-30ui12hwhunzoj200axhcaNAIROBI, KENYA

ALIYEKUWA beki wa timu ya Ulinzi Stars ya nchini Kenya, Kevin Ouma ‘Oush’, amepoteza maisha kwa kuuawa na Al Shabab nchini Somalia.

Oush alikuwa beki kisiki wa pembeni wa klabu ya Ulinzi Stars ambaye aliisaidia timu hiyo kushika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Gor Mahia mwaka 2015.

Mbali na kuwa mchezaji wa klabu hiyo, pia alikuwa ni askari wa Taifa hilo, huku akiwa miongoni mwa askari ambao walikuwa nchini Somalia kwa ajili ya kulinda amani dhidi ya Al Shabab, ila mchezaji huyo alipoteza maisha kutokana na shambulio la kigaidi ambalo liliua zaidi ya askari 100 Januari, mwaka huu.

Hata hivyo, mchezaji huyo alitambulika kutokana na vipimo vya DNA, baada ya namba ya kombati yake kupotea.

Klabu ya Ulinzi Stars imesikitishwa na kifo cha mchezaji huyo na kudai kwamba wapo pamoja na familia ya marehemu kwa kipindi hiki kigumu cha msiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles