25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Katty Collection inavyoadhimisha miaka 10 kwa kuinua mabinti

NA JEREMIA ERNEST, Mtanzania Digital

Katty Collection ni kampuni inayojihusisha na mitindo hasa mavazi ya Kiafrika. Ilianzishwa na mbunifu Titty Morris ambaye mwishoni mwa wiki hii anatarajia kusherehekea miaka 10 tangu alipoanzisha kampuni hiyo.

Kama ilivyo kwa taasisi na kampuni nyingine, kuadhimisha kumbukumbu ya kuanzishwa kwake kwa matukio mbalimbali, Katty Collection imeamua kusheherekea kwa kugawa cherehani za kushonea nguo 100 kwa mabinti na vijana ili kuwainua katika tasinia ya mitindo

Sherehe za kumbukumbu ya miaka 10 ya kampuni hiyo itafanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam ikitarajiwa kuhudhuriwa na wanamitindo na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo, huku mgeni rasmi akiwa ni Katika sherehe hiyo mgeni rasm atakuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Mmiliki wa kampuni hiyo Titty, anasema pia kutakuwa na onyesho la mavazi kutoka kwa wabunifu watatu chipukizi na Katty Collection yaliyotamba tangu kuanzishwa kwake.

Anasema katika sherehe hiyo, atazindua mpango wa kusaidia mabinti na vijana wanaotaka kuanza kujikita katika tasnia ya mitindo lengo ikiwa ni kurudisha kile alichokipata kwa jamii.

“Nitatoa cherehani 100 kwa wanawake na vijana ambao wanachipukia katika tasnia hii ambao hawana mtaji, mpango huu nitaufanya ndani ya miaka mitano, nitauzindua rasm katika sherehe hii,” anasema Titty.

Mafanikio na changamoto ndani ya miaka 10

Anasema ndani ya miaka 10 mafanikio makubwa ikiwamo tuzo mbili za mbunifu bora wa mwaka 2021 katika tamasha la Swahili Fashion Week na Pawes Awards Women in Fashion and Beauty 2022 aliyotunukiwa nchini Afrika Kusini.

Aidha amefanya kazi na watu mbali mbali kama vile wasanii wa kubwa miongoni mwao ni Naseeb Abduli ‘Daimond’ na Reyvan katika wimbo ya ‘Salome’, pia Lavalava na Hamonize.

Tuzo

Anaeleza kuwa changamo ni mlipuko wa virusi vya Corona kwa sababu wateja wake wengi wanatoka nchi za nje na wengine ni Watanzania ambao wapo maofisini ambao walianza kufanya kazi nyumbani.

“Nina wateja kutoka nchi za nje kipindi cha Corona niliwakosa na wengine Watanzania walikuwa wanafanya kazi nyumbani, harusi nazo zilisitishwa ilikuwa ni kipindi kigumu kwangu,” anaeleza.

Neno lake kwa wabunifu Watanzania

Anasema wabunifu wengi hawapendi kujitangaza katika kazi zao, wamekua waoga kutumia kazi zao wakati wana vipaji vikubwa.

Ameeleza kuwa yeye amefanikiwa kwa sababu asilimia 80 ya nguo anazo vaa ameshona mwenyewe, hii ni njia kubwa ya kujitangaza bila hata ya kutumia gharama kubwa.

Pia amesisitiza wabunifu kutobadili majina yao wanayoanzia kazi na kubaki katika jina moja ili kutoyumbisha wateja, pia kuweka nembo kwenye vitendea kazi vyao ikiwamo vifungashio vya nguo kwa wateja na kutumia vizuri mitandao ya kijamii.

Anasema hapa nchini anawakubali wabunifu Ally Rehmtula na Binjuu kwa sababu wanajituma katika kazi japo wapo wengi ambao nao anawapenda.

Aidha amesema nguo za wabunifu zinakuwa bei ya juu kutokana na mazingira ya kazi kwa mfano, wanalipa kodi , kulipia leseni ya biashara, kujisajili Basata, ila mafundi wa kawaida unakuta ameweka cherehani kibarazani halipi kodi hata kama ubora wa nguo utakuwa sawa bei haziwezi kufanana.

Kwa nini Katty Collection?

Akizungumzia jina la Katty Collection, Titty, anasema ni muunganiko wa herufi za majina ya watoto wake wawili wa kike pamoja na jina lake.

“Wakati natafuta jina nilichukua herufi zinazopatikana katika majina ya mabinti zangu wawili kwa sababu nilipokuwa naanzisha hii biashara nilikuwa nashauriana nao kila hatua hadi leo wanafahamu kila kitu kinachohusu ofisi hii hata nisipo kuwepo wanaweza kuendesha ikasimama imara,” anasema Titty.

Aweka wazi mapenzi yake na muziki

Anasema kwa sasa wimbo anaoupenda ni ‘Mtasubiri’ ulioimbwa na Daimond na Zuchu.

Pia anapenda kuogelea na shabiki wa soka kwa hapa nchini akishabikia timu ya Simba.

Pamoja na mitindo, taaluma yake ni uhasibu amefanya kazi katika kampuni na taasisi mbalimbli baada ya kuacha kazi akaamua kujikita katika ujasiriamali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles