26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kassim awataka wasanii kuipenda nchi yao

kASSIM-mGANGANA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Kassim Mganga, amesema hoja ya wasanii kwenda nje ya nchi kufanya kazi zao kwa kigezo cha kutafuta mazingira tofauti ni hoja dhaifu, kwa sababu Tanzania kuna mazingira mazuri ambayo huwezi kuyapata popote pale.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kassim alisema Waafrika hivi sasa wamebadilika wanataka kuona mazingira yao yakitangazwa kama vile visiwa, milima na pwani mbalimbali ndiyo maana video ya Nasema nawe wimbo wa Diamond Platnumz umeshinda tuzo ya video bora ya mwaka kwenye Tuzo za AFRIMA.

“Tanzania tuna mazingira mazuri ambayo nchi nyingine za Afrika hayapo na yanavutia kweli kweli, nawashauri wasanii ni bora wakawaita waongozaji wa video wa nje wakaja kufanya video zao kwenye mbuga, pwani na mazingira mengine yatakayoitangaza nchi yetu,” alisema Kassim.

Aliongeza kuwa video ya wimbo wake wa Subira aliomshirikisha Christian Bella, ameifanya kwenye mazingira ya Bagamoyo pamoja na ufukwe wa Ununio jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles