25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kanye West ampa Kim bonge la zawadi

Grand Opening of RYU Restaurant - InsideNEW YORK, MAREKANI

BAADA ya Kim Kardashian na Kanye West kupata mtoto wao wa pili ‘Saint’, mkali huyo wa hip hop ameamua kumpa zawadi mke wake ya Sh bilioni 2.

Msanii huyo ameamua kuonesha jeuri ya fedha ikiwa ni shukrani kwa mke wake kwa ajili ya kumzalia mtoto wa pili.

Kanye alifanya hivyo ikiwa ni siku chache tangu Kim ajifungue mtoto huyo ambaye kwa sasa amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa Jarida la People la Marekani, limeandika kwamba Kanye amekuwa mtu wa furaha kubwa tangu ujio wa mtoto wake huyo na kwamba amekuwa akimhudumia Kim kama vile malkia.

“Tangu Kim amejifungua amekuwa ni mchovu sana kwani bado ana maumivu makali ndiyo maana Kanye anafanya kila aliwezalo na kumsaidia kila kitu kama malkia anavyofanyiwa,” iliandika sehemu ya jarida hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles