BAADA ya Meek Mill kumvisha pete mpenzi wake Nick Minaj, wawili hao wamepanga kufunga ndoa mwakani.
Kupitia mtandao wa Instagram, mkali huyo wa hip hop, Minaj alisema kuvishwa pete ni dalili ya harusi kukaribia.
“Baada ya Mill kunivisha pete najua kwamba watu wana maswali mengi ambayo hayana majibu, lakini ukweli ni kwamba hii ni dalili ya harusi kukaribia.
“Nampenda sana Mill na ninaamini ananipenda na ndio maana amenivisha pete, kila kitu kitakuwa hadharani mwakani, mipango yetu mikubwa kwa sasa ni kufunga ndoa ifikapo 2016,” aliandika Minaj.