26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

KARRUECHE ADONDOSHA CHOZI NIGERIA

image-7ABUJA, NIGERIA

ALIYEKUWA mpenzi wa msanii wa RnB nchini Marekani Chris Brown, Karrueche Tran, amejikuta akidondosha chozi baada ya kukutana na watoto yatima nchini Nigeria.

Mrembo huyo alikuwa nchini humo kuongoza sherehe za Pool Party mjini Abuja, lakini aliamua kutembelea kwenye
kituo cha watoto yatima cha IDP Camp, ambapo aliwakuta watoto hao wakiwa wamevaa T-shirt zilizoandikwa
‘Bring Back Our Girls’ (‘Wasichana wetu warudishwe’) Inakumbukwa kuna wasichana wengi ambao wametekwa nchini humo ambapo hadi sasa hawajulikani walipo, hivyo alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akidondosha chozi.

“Watoto wengi wa Nigeria wanaonekana kuguswa na tukio la utekaji, nilijikuta nikidondosha chozi baada ya kuwasikia wakielezea juu ya tukio hilo la utekaji, lakini nilifurahi sana kuzungumza na watoto hao.

“Nimejifunza mengi kutoka kwao na watu wa Nigeria kwa jumla, tayari nimekuwa na uzoefu wa maisha ya Afrika,
nitajaribu kusaidia Afrika kutokana na uwezo wangu nikisaidiana na wadau mbalimbali,” alisema Karrueche.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles