Kanye West awaomba radhi Wiz Khalifa na Amber Rose

0
705

2015 MTV Video Music Awards - Fixed ShowNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, amewaomba radhi, Wiz Khalifa na mama mtoto wake, Amber Rose, baada ya kuwashambulia kwa maneno makali.

Licha ya maneno hayo kutafsiriwa kuwa makali, pia Kanye alisema kuwa Wiz Khalifa asingeweza kumpata Amber na kuzaa naye mtoto kama asingeachwa naye.

Hata hivyo, Wiz hakujibu lolote juu ya kauli hiyo, lakini Amber alijibu kwa kumtaka asimhusishe mtoto wake katika mgogoro wao binafsi.

“Najua nitakuwa nimewakosea sana Wiz Khalifa na Amber Rose, sitamzungumzia mtoto wenu tena, nawapenda wote na nawatakia heri,” Kanye aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

 

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here