26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Chris Brown adaiwa mtoto

Nia GuzmanNEW YORK, MAREKANI

MAMA wa mtoto wa Chris Brown, Nia Guzman, amedai mtoto wake kutoka kwa msanii huyo kwa madai kwamba anamtesa na moshi wa sigara unaomsababishia ugonjwa wa pumu.

Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja (Royalty), anaishi na baba yake, lakini mama wa mtoto huyo amedai kwamba mwanawe anateseka na ugonjwa wa pumu ambao unasababishwa na moshi wa sigara.

“Ninamuonea huruma mwanangu, mara ya mwisho kukutana naye nilishangaa sana baada ya kuhisi harufu ya moshi wa sigara.

“Hata hivyo, mbali na moshi wa sigara, pia kwa sasa ana matatizo ya pumu inayotokana na moshi huo, hivyo ninahitaji kuwa na mwanangu nimlee mwenyewe,” alisema Guzman.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles