MSANII wa muziki nchini Uingereza, David Bowie, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 69, baada ya kusumbuliwa kwa ugonjwa wa kansa.
Bowie ambaye alikuwa anafanya muziki na filamu alikuwa anasumbuliwa na kansa kwa kipindi kirefu, hata hivyo wiki iliyopita alisherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa hospitali kabla ya kupatwa na umauti.
Kampuni ya filamu ya Hollywood ya nchini Marekani, imethibitisha kutokea kwa kifo cha msanii huyo kupitia akaunti yao ya Facebook.
“David Bowie amefariki baada ya kupigania maisha yake kwa mwaka mmoja na nusu kutokana na kusumbuliwa na utgonjwa wa kansa, tunamtakia apumzike kwa amani na tunaipa pole familia yake hasa katika kipindi hiki
kigumu,” waliandika kupitia mtandao huo.
Msanii huyo amefariki huku akiwa tayari ameachia jumla ya albamu 25, huku akitamba na nyimbo zake kama vile ‘Space Oddity,