26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Kangi Lugola amshambulia Lowassa

IMG_0143Na Ahmed Makongo, Mwibara

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Mwibara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kangi Lugola, amemshambulia kwa maneno makali mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, kuwa umati wa watu wanaofurika kwenye mikutano yake haumaanishi kumkubali isipokuwa una sababu zaidi ya hiyo.

Lugola aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, uliofanyika Uwanja wa Kata ya Kisorya katika Jimbo la Mwibara, mpakani mwa wilaya ya Bunda na Ukerewe iliyoko Mkoa wa Mwanza.

Lugola alisema watu wasishangae umati mkubwa anaoupata Lowassa kwenye mikutano yake ya kampeni kwa sababu wananchi wengi sio kwamba wanamkubali bali wanakwenda kuangalia na kushangaa mambo mengine.

Alisema wakati wa mchakato wa kuomba ridhaa ya kugombea urais ndani ya CCM alishawishiwa na aliowaita wapiga debe wa stendi kumuunga mkono Lowassa na kupanda basi lake ambalo lilikuwa bovu.

“Watu watasema kwamba mbona nilikuwa kwake, unajua wapiga debe hao ni watu hatari sana, ni kama hao wa kwenye hiace, ukifika hapo stendi watakuvuta huku na huku wakisema gari zuri ni hili…..sasa nilipanda basi la Lowassa, kufika njiani likaharibika nikapanda basi zima la Dk. John Pombe Magufuli na sasa ninakwenda nalo mbele kwa mbele,” alisema Lugola.

Lugola alisema kiongozi anayefaa kuwa rais kati ya wagombea wote wanane wa nafasi hiyo ni Dk. Magufuli, kwa sababu afya yake ni imara na pia anao uwezo mkubwa wa kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles