33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Shein aahidi kuboresha elimu Pemba

imageNa Esther Mbussi, Zanzibar

MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Mohamed Shein, ameahidi kutoa kompyuta na kuongeza idadi ya walimu wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari Kusini Unguja.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni eneo la Paje, Kusini Unguja Dk. Shein alisema kuongeza idadi ya walimu wa masomo ya sayansi kutasaidia kuongeza ufaulu wa masomo hayo.

“Serikali itaboresha sekta ya elimu kwa kujenga shule na tayari tunamalizia shule 22 tulizoanza kujenga mwaka jana. Tumefanikiwa kutekeleza ahadi zetu tulizoahidi, tuliahidi maji tumefanikiwa lakini hapa Paje kwa bahati mbaya wafadhili wetu hayajakamilisha ila jitihada za kuleta maji Paje zinaendelea,” alisema Dk. Shein.

Kuhusu uchimbaji wa mafuta na gesi, Dk. Shein alisema wamekubaliana na Rais Jakaya Kikwete kuwa Tanzania Bara iendelee kuchimba mafuta yake na Zanzibar itachimba ya kwake.

“Aidha, tulikubaliana Zanzibar tutunge sheria yetu wenyewe, tayari tumeshaandaa na rasimu iko tayari, nitakaporudi nitachimba mafuta ndani ya miaka mitatu,” alisema Dk. Shein.

Awali, aliyekua Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, alisema anawashangaa viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kulalamika kuwa Serikali haitoi ajira wakati Wizara ya Ajira ilikua chini ya uongozi wao.

Alisema katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), Wizara za Ajira, Biashara, Utalii, Viwanda, Viwanja vya Ndege na Barabara zilikuwa zinasimamiwa na mawaziri wa CUF.

“Anapotokea mpinzani anayesema Serikali ya CCM haitoi ajira huyo apimwe akili… ningekuwa mimi ndiye Maalim Seif ningewaita mawaziri wangu nikawauliza kimetokea nini lakini wao kila mtu ni kulalamika tu, haijulikani kiongozi nani.

“Ukiwauliza kwanini mnashindwa wanasema sera inayotekelezwa ni ya CCM, lakini kazi ya upinzani ni kutoa mawazo na kutengeneza sera mbadala, binafsi nilichokitegemea kwa wenzetu hao kimekuwa tofauti,” alisema Vuai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles