30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Lubuva amshangaa Mbowe

Pg 4 oct 3Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa Uchaguzi nchini Jaji Mstaafu Damian Lubuva, ameeleza kushangazwa na kauli zinazotolewa na baadhi ya vyama vya siasa wakiwahamasisha wafuasi wao hasa kundi la vijana kubaki vituoni ili kulinda kura.

Kauli hiyo ya Lubuva ambayo aliitoa Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari inaonekana kumjibu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

Akihutubia mkutano wa kampeni jijini Dar es Salaam juzi katika viwanja wa Kawe, Mbowe aliwataka wanachama na wafuasi wao kubaki vituoni siku ambayo watapiga kura ili kuzilinda zisiibiwe.

Hata hivyo, Jaji Lubuva alisema kauli hiyo inajenga mazingira ya kuleta fujo nchini.

“Nashangazwa na kauli hizo kwa sababu Tume tulishasema kwamba mfumo tulioandaa ni mzuri na umeboreshwa kwa kuzingatia maoni yao… inakuwaje tena wanaendelea kuwahamasisha wafuasi wao hasa vijana wabaki vituoni kulinda kura kwanini… mawakala wapo kwa ajili gani,” alihoji.

Jaji Lubuva alisema NEC inasisitiza watu watakaokuwa wamekwisha kupiga kura kuondoka vituoni kwani endapo vijana watabaki kuna uwezekano wengine wakapata hofu ya kwenda kupiga kura.

“Ndio maana tunawataka waondoke lakini hawa wanasiasa wanaosema wabaki kulinda kura huenda wana ajenda yao maana wasiwasi wa nini,” alihoji Jaji Lubuva.

Aliwataka watazamaji wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kipindi chote cha usimamizi bila kufungamana na upande wa chama chochote cha siasa.

Aliwataka wanawake nchini kuhimiza amani kipindi hiki cha uchaguzi kwani wana nguvu kubwa ya ushawishi ambayo inaweza kuzuia vurugu zisitokee.

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa mada katika semina iliyowakutanisha NEC na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wanawake nchini Kaimu Mkurugenzi wa Sheria NEC, Emmanuel Kawishe, alisema NEC imejipanga  kusimamia vizuri Uchaguzi Mkuu kwa kuhakikisha unakuwa huru na haki.

“Tumeandaa mfumo mbadala ujulikanao kama ‘Spreadsheet Excel RMS’ ambao utatumika kuondoa makosa mbalimbali ya kibinadamu yatakayojitokeza katika zoezi la ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi,” alisema.

Kawishe alisema mfumo huo utatumika iwapo kutakuwa na changamoto katika kutumia mfumo ulioandaliwa.

“Tume imeandaa mfumo wa menejimenti ya matokeo (Result Management System) ambao utatumika kuondoa makosa mbalimbali ya kibinadamu yanayoweza kutokea kwa bahati mbaya katika ujumlishaji wa matokeo.

“Kasoro au makosa hayo ni kama ujumlishaji wa kituo kimoja mara mbili, kukosea uandikaji wa 7 badala ya 1, usahihi wa ujumlishaji na mengineyo, mfumo huu si mgeni kwani ulitumika katika uchaguzi wa 2005 na 2010.

“Kwa uchaguzi wa mwaka huu, tumefanya uboreshaji na kuondoa mapungufu katika maeneo yote yaliyokuwa na changamoto 2010 na tumeandaa mfumo huu mbadala ambao utatumika kama huu uliopo utakuwa na changamoto,” alisema.

Alisema katika usimamizi wa zoezi la uchaguzi tume imepata changamoto ikiwamo ya kufariki kwa baadhi ya wagombea pamoja na kuongezwa kwa mipaka ya kiutawala ambayo imeanzishwa baada ya kutangazwa kwa majimbo mapya.

“Kuna baadhi ya kata mpya zimeanzishwa ambazo ni Ifakara, Bariadi, Kishapu na Bulyanhulu wakati Tume ikiwa tayari imetangaza majimbo, hivyo zipo katika tishio la kutopiga kura lakini suala hilo linashughulikiwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,391FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles