25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya Samsung yazindua kifaa kipya

 Makamu wa Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya vifaa vya  elektroniki ya Samsung Afrika Mashariki, John Park
Makamu wa Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya vifaa vya elektroniki ya Samsung Afrika Mashariki, John Park

Na MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Kielektroniki ya Samsung Afrika Mashariki, imezindua kiyoyozi kipya chenye vifaa vya 360 Cassette, DVM Chiller, Next generation DVM S 30 HP pamoja na kifaa cha pembeni cha kutolea hewa VRF unit.

Mbali na vifaa vipya, Samsung imekua moja ya kampuni inayoongoza kwenye sekta hiyo kutokana na uzoefu wake wa kipekee, ubora wa bidhaa zake pamoja na utoaji wa huduma bora.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam juzi, Makamu wa Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya vifaa vya  elektroniki ya Samsung Afrika Mashariki, John Park,  alisema kutokana na hali ya joto kuongezeka kwa kiasi kikubwa, viyoyozi vimekua kama vifaa muhimu badala ya kuonekana kama ni anasa katika maisha.

“Na hii imetupelekea sisi kutambulisha kiyoyozi ambacho kinafanya kazi kwa ufanisi zaidi, huku ikitumia fedha kidogo sana kuiendesha,” alisema.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wabunifu wa Majengo Tanzania, Mhandisi Henry Mwoleka, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alisema teknolojia inavyokuwa, wabunifu katika sekta mbalimbali wanagundua vitu au vifaa vinavyotumika.

Alisema awali kulikuwa na viyoyozi vilivyokuwa vikifyonza hewa kutoka nje na kuingiza ndani, lakini baadaye zimekuja nyingine ambazo zinatoa hewa zinazopoza bila kuathiri upande mwingine.

“Lakini kifaa hiki kipya kinaonekana kutoa hewa ambayo inahitajika kwa usawa sehemu zote, hivyo sisi wabunifu wa majengo tunazihitaji kwa sababu zinachukua nafasi ndogo lakini pia zina ubora wake,” alisema.

Aliwataka wabunifu majengo kuangalia ubora wa bidhaa hizo ili waweze kuzitumia na wanapaswa kuachana na bidhaa feki ambazo hazijathibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) au vyombo vingine vya ubora vya kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles