24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Asilimia 90 ya makazi Ilemela hayajapimwa

 Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Na CLARA MATIMO-MWANZA

ASILIMIA 90 ya eneo la Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza, haijapimwa ingawa wananchi wake wanaishi katika makazi yaliyoendelezwa.

Hayo yamebainishwa jijini Mwanza jana na  Meneja Mradi wa Uboreshaji Nyumba na Makazi Wilaya ya  Ilemela unaotekelezwa na Shirika lisilo la Serikali la TAHEA kwa ufadhili wa W-Effect  la nchini Sweden, Musa Masongo, wakati akizungumza katika kongamano la kujadili fursa ya utawala mpya katika kumiliki ardhi na changamoto zake.

Alisema Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,  katika  hotuba yake ya bajeti 2016/17  kwa kutambua changamoto zilizopo katika sekta ya wizara yake.

Lukuvi aliziagiza halmashauri zote na wataalamu washushe  ramani  za mipango miji katika ngazi ya mitaa  ili wananchi wajue ni nini kimepangwa kujengwa  katika maeneo wanayotaka kujenga, lakini hadi sasa halijatekelezwa kikamilifu.

“Hebu fikiria mwananchi huyu ninayemzungumzia ni wa kipato cha chini kuelekea cha  kati ambaye kipato chake kwa siku ni Sh 5,600 anajinyima anajenga nyumba katika eneo ambalo halijapimwa baada ya muda anaambiwa hapo alipojenga si makazi ya watu anabomolewa halafu halipwi fidia kwa wakati jamani huu umaskini tutapambana nao vipi?,” alihoji Masongo na kuongeza.

“Tumeandaa kongamano hili ili kukutana na   wenyeviti wa mitaa na watendaji wa kata jumla 50 lengo ni kujadili fursa  zilizopo katika  utawala huu wa awamu ya tano kwenye  suala zima la kumiliki ardhi na changamoto zake,” alisema.

Alisema kama mwananchi  hana ardhi iliyorasimishwa hawezi kuwa rafiki wa benki kwa kuwa ili kupata mkopo lazima awe  na dhamana, hivyo dhamira ya serikali ya kuboresha maisha ya watu wake inaweza ikatekelezwa kwa urahisi endapo watapimiwa ardhi na kumilikishwa rasmi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,476FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles