IS yapoteza robo ya maeneo inayodhibti

0
887

isis-black-700x394

DAMASCUS, SYRIA

UTAFITI uliofanywa na taasisi ya wachambuzi wa masuala ya ulinzi, unasema kundi la wapiganaji lijiitalo Dola la Kiislamu (IS), limepoteza zaidi ya robo ya eneo lililokuwa likiidhibiti.

Ripoti hiyo inasema kuwa eneo hilo limepungua kwa asilimia 28 tangu kundi hilo lianze kushambulia na kudhibiti maeneo hayo mwaka 2015.

Kundi hilo kwa sasa linadaiwa kudhibiti eneo lenye ukubwa wa taifa la Siri-Lanka pekee.

Wachambuzi hao wanasema ijapokuwa kasi hiyo ya kupoteza maeneo inayodhibiti imepungua miezi mitatu kabla ya Oktoba, maeneo hayo ni pamoja na maeneo muhimu karibu na mpaka wa Uturuki, mji wa Syria wa Manbij na kambi moja ya Jeshi la angani kusini mwa mji wa Mosul nchini Irak.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here