28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya Kilombero yaibuka kidedea tuzo za ATE 2022

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Sukari ya Kilombero imefanikiwa kunyakua tuzo katika kipengele cha cha Uanagenzi na Mafunzo (Apprenticeship and Internship) huku ikishika nafasi ya pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) na kupokea cheti cha shukrani kwa kudhamini hafla hiyo wakati wa tuzo za zitolewazo na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika 2022 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu (kulia) Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo Meneja wa Maghala wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero (kushoto), Anthony Rweyemamu baada ya Kampuni kushinda nafasi ya pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Desemba 2, 2022 ambapo kampuni ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kilombero Sugar Company Limited wakiwa katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika Desemba 2, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City. Kampuni hiyo ilitajwa kuwa mshindi wa kipengele cha Uanagenzi na Mafunzo, na Mshindi wa pili katika kipengele cha Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content) na kupokea cheti cha shukrani kwa kudhamini hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Masuala ya Biashara- Bruno Daniel , Mkuu wa Rasilimaliwatu Idara ya Kilimo – Cleopatra Nasari, Meneja wa Maghala Dsm/Morogoro Anthony Rweyemamu na Mtafiti wa Masoko, Lenin Rugaimukamu.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles