30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Bunge yampa mbinu RC Mwanza kutatua changamoto ya miundombinu

Na Clara Matimo, Mwanza

Kamati ya Kudumu ya bBunge ya Miundombinu leo Machi 14 imeanza ziara yake mkoani Mwanza kukagua na kujiridhisha na utekelezaji wa miradi ya Kitaifa inayoendelea mkoani hapa.

Caption: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel,(hayupo pichani)katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkoa huo akiwa ameongozana na wajumbe hao nao hawapo pichani kabla hawajaanza ziara ya kukagua miradi ya kitaifa mkoani humo.Picha na Clara Matimo

Akizungumza katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, Mwenyekiti wa  kamati hiyo, Seleman Kakoso, amemshauri mkuu huyo wa mkoa kutembelea hiyo ili abaini changamoto mbali mbali zilizopo.

Pia amesema wamekuwa wakisikia changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wafanyakazi hasa wa ngazi za chini kutopata stahiki zao  ambapo ameahidi kujiridhisha na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo.

“Tunaenda kufanya kazi ambayo inamalengo makubwa ya kuisimamia serikali pale ambapo tutabaini changamoto za miradi tutakwambia nini kifanyike lakini ushauri wangu wa awali  fika kwenye miradi maana ili na wewe ujiridhishe.

“Wakandarasi wanalipwa fedha nyingi sana na serikali wajibu wetu wabunge ni kuhakikisha wanatoa huduma za kijamii kwenye jamii husika ili waache kitu ambacho kitakuwa na manufaa kwa wananchi wa mkoa huu baada ya ujenzi wa miradi hiyo kukamilika ikiwemo ujenzi wa reli,”ammesema Kakoso.

Kwa upande wake, Mhandisi Gabriel akizungumzia utekelezaji wa anuani za makazi amesema wamevuka lengo kwa kutambua nyumba  653,827 sawa na asilimia 118.54.

“Lengo la mkoa ilikuwa ni kufikia nyumba 551, 554 hadi  Machi 13 mwaka huu lakini hadi sasa  jumla ya namba ambazo zimeishawekwa ni 653,827   lengo letu ni kuhakikisha mwezi huu tunamaliza kila kitu kwa sababu agizo la Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani alilolitoa Februari 8 mwaka huu ni amri halijadiliwi kwenye kikao chochote kile kufanya hivyo ni usaliti hivyo baada ya agizo hilo tulianza utekelezaji.

“Mheshimiwa mwenyekiti naomba nikuhakikishie kuwa miradi yote ya umma inayotekelezwa ndani ya mkoa huu hautasikia tumelalamika,ikitokea mtumishi yeyote wa umma anafanya ubadhilifu wa kuihujumu utasikia yuko mahakamani,  jela, takukuru au anafilisiwa, ndani9 ya mkoa huu niao uongoza mambo ya ubadhilifu, uzembe, uvivu,  ni mwiko, tunaendelea kutoa elimu na maombi, maombi yanavunja nguvu za uovu, elimu inaongeza maarifa  kwenye vichwa ili tukichukua hatua tujue tumemshirikisha Mungu na serikali,”amesema na kuongeza.

“Tumejipanga kulinda heshima ya bunge, serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, tunachozungumza ndicho tunachokiishi na kukitenda tunaamini tuitaongoza katika kutekeleza agizo hilo kati ya mikoa yote haoa nchini,”ameeleza Mhandisi Gabriel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles