30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati: Wafugaji wapatiwe elimu namna bora ya uchunaji ngozi

Safina Sarwatt, Kilimanjararo

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imetembelea kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha Kilimanjararo International Leather kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro, nakushauri elimu itolewe kwa wafugaji juu ya uchunaji wa ngozi bora na utunzaji ili waweze kupata soko la uhakika za bidhaa zao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Najma Murtaza Giga ametoa ushauri huo wakati wa ziara ya kamati hiyo kiwandani hapo ambapo amesema mradi huo ni mkubwa hivyo kuwataka jeshi la magereza ambao ndiyo wasimamizi wa kiwanda hicho kuhakikisha kiwanda hicho kinakuwa endelevu.

Aidha ameishauri uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora ili kupata masoko ya uhakika wa bidhaa zake ndani na nje ya nchi.

Naye Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro, Joseph Tadayo akitoa ushauri wake amesema uwepo wa mradi huo ni Mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kwamba utazalisha ajira nyingi huku akiwashauri kuanzisha miradi mingine kama huo katika Mikoa mingine.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF ambao ni wabia katika mradi huo Mhandisi Hosea Kashimba amesema ujenzi wa awamu zote za mradi wa kiwanda hicho ukikamilika itatoa ajira 3,000 za kudumu na ajira 7,000 ambazo siyo za kudumu.

Amesema kuwa kukamilika huo pia utapelekea kuzalisha viatu jozi million mbili za viatu pamoja na bidhaa nyingine za ngozi zaidi ya 180,000 ikiwemo mikanda ya ngozi, mabegi, makoti na pochi za kiume na za kike.

Mwakilishi wa Kamishana wa Magereza, Sacp Justin Kaziulaya amesema kuanzishwa kwa kiwanda cha ngozi miaka ya 70 kumewezesha jeshi la magereza kuwapa wafungwa ujuzi ila tu halina uwezo wa kuwapa vifaa na mitaji wamalizapo vifungo vyao waweze kujiajiri na hivyo kupunguza wimbi la uhalifu nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles